SHOW / EPISODE

7. Ujumbe wa DYFEM kuhusu Zahabu Safi pa Bikenge Jimboni Maniema inchini Kongo

3m | Nov 10, 2023

[Musique]

Mtangazaji:

Taarifa! Taarifa!

Hakuna watoto katika eneo la uchimbaji wa dhahabu.

Watoto wanapaswa kulindwa kutokana na kazi yoyote hatari, ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa dhahabu.

Hakuna wanawake wajawazito katika eneo la uchimbaji wa dhahabu.

Wanawake wajawazito wanapaswa kulindwa kutokana na hatari yoyote kwa afya zao na afya ya mtoto wao.

Hakuna matumizi ya kemikali hatari katika uchimbaji wa dhahabu.

Matumizi ya kemikali hatari kama vile zebaki yaani mercure yanapaswa kuepukwa, kwani zinadhuru afya ya wafanyakazi pia ina aribu mazingira.

Haiko vizuri kunywa pombe kali katika maeneo ya migodi yaani nafasi ya kuchimba madini.

Unyanyasaji, kwa aina yoyote ile, unapaswa kuepukwa katika maeneo ya uchimbaji wa dhahabu.

DYFEM inawaita wote wanaohusika na secta ya uchimbaji na ununuzi wa dhahabu katika eneo la Kasongo/Bikenge kuheshimu kanuni hizi ili kuwe dhahabu safi. 

Vyama vya ushirika vya madini vinapaswa kushirikiana na jamii za mitaa ili kusaidiya kuelekeya kwenye uchimbaji madini unayoheshimika. Hii inaweza kusaidiya jamii inayo kuwa kwenye hatari ya kazi mbali mbali za uchimbaji madini ili wapate kufuata majukumu yao.

Vyama vya ushirika vya madini ambavyo vinataka kutekeleza hatua za kulinda wanawake na watoto zapashwa :

  • Anza kwa kuchunguza hatari za kazi ya uchimbaji madini. Hii itasaidia kutambua maeneo ambapo hatua za ulinzi zinahitajika.
  • Kusaidiya sheria kutimizwa na kuleta zaidi uwazi ndani ya secta ya madini. Hizo sheria zapashwa julikana na wanamemba wote wa ushirika.
  • Kufundisha wanamemba wa ushirika kuhusu sera na taratibu mpya. Hii itahakikisha kwamba kila mtu anajua sheria na matarajio.
  • Kuanzisha mipango ya kuchunguza kama kila hatua ina heshimika ndani ya secta ya uchimbaji wa dhahabu.

[Musique]

DYFEM, kwa dhahabu ya kimaadili.

Huu ni ujumbe kutoka kwa Dynamique des Femmes de Mines DYFEM katika mradi wake “Promotion de la mise en œuvre du devoir de diligence en territoire de Kasongo en province du Maniema sous le financement de Global communities dans son projet Zahabu SAFI financé par USAID” katika eneo la Kasongo katika mkoa wa Maniema chini ya ufadhili wa Global Communities katika mradi wake wa Zahabu SAFI unaofadhiliwa na USAID".

[Musique]

Audio Player Image
Tetea Mazingira Swahili Podcast
Loading...